Connect with us

Soka

Alonso,Mourinho Kumrithi Zidane Madrid

Rais wa klabu ya Real Madrid Frolentino Perez inadaiwa yuko mbioni kumtimua kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane kufuatia matokeo yasiyoridhisha licha ya usajili kabambe iliofanya timu hiyo katika dirisha la usajili la majira ya joto msimu huu.

Real Madrid iliwanasa Eden Hazard kutoka chelsea kwa dau la paundi milioni 100 na ushee huku ikimsajili Elder Militao kutoka Fc Porto ya Ureno huku Luca Jovic kutoka Frankfurt ya ujerumani huku wakongwe kama Sergio Ramos,Luca Modric na Dani Carvahal wakisalia kikosini licha ya tetesi za kuhama.

Timu hiyo wiki hii imepoteza mchezo muhimu wa Uefa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Paris st.Germans ya Ufaransa huku staa wa zamani wa timu hiyo Angel Di Maria akifunga mabao mawili.

Kufuatia matokeo hayo ya kusuasua hasa katika la liga ambapo timu hiyo imecheza michezo minne na kushinda miwili huku wakitoa sare michezo miwili wakiwa na pointi nane mbili nyuma wa vinara wenye pointi kumi.

Perez anafikiria kumuajiri kocha wa zamani wa timu hiyo Jose Mourinho ama Xabi Alonso endapo timu hiyo itaendelea na matokeo mabovu katika mechi zinazofuatia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka