Connect with us

Soka

Samatta Kibaruani Uefa

Nahodha wa Taifa stars Mbwana Samatta kesho ataweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza Uefa ambapo atakuwa uwanjani na timu yake ya Krc Genk kucheza mchezo wa klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Redbull Salzburg ya Australia.

Genk italazimika kusafiri mpaka nchini humo kucheza mchezo huo utakaofanyika katika uwanja wa Red bull Arena wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 30188 uwanja ambao ulifunguliwa rasmi mwaka 2003.

Hata hivyo Genk inabidi wajipange dhidi ya Selzburg maana wameshinda michezo yao yote saba waliyocheza katika ligi kuu ya nchini mwao huku Genk wakitoka kupoteza mechi ya mwisho waliyocheza kwa mabao 2-1 dhidi ya charleloi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka