Connect with us

Soka

Hapatoshi Stars na Burundi Kesho

Timu ya soka ya Tanzania (Taifa stars) kesho itavaana na Burundi katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia nchini qatari mwaka 202 mchezo ambao utafanyika katika uwanja wa taifa nchini.

Mchezo huo wa marejeano baada ya ule wa awali ulifanyika nchini humo na matokeo kuwa sare  ya 1-1 ambapo leo mshindi lazima apatikane ili kwenda hatua inayofuatia ya michuano hiyo.

Stars itategemea zaidi hamasa ya mashabiki baada ya shirikisho la soka nchini(Tff) kuweka kiingilio cha shilindi elfu mbili ili kuvutia mashabiki wengi kuingia uwanjani.

Mbwana Samata anayeichezea Krc Genk ya nchini Ubeligiji ndio anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya taifa stars huku Saido Berahino akisaidIwa na Cedrick Amis watakua  na kazi ya kuwazidi maarifa Kelvin Yondani na Erasto Nyoni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka