Connect with us

Soka

Kejeli Zamponza Zahera

Licha ya kupigwa faini na bodi ya ligi baada ya kutovaa nadhifu,Kocha wa Yanga sc Mwinyi Zahera amefungiwa kutokaa katika benchi la timu hiyo katika mechi tatu mfululizo.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya kocha huyo kutoa maneno ya kejeli kwa bodi ya ligi wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya Ruvu shooting ambapo timu yake ilipoteza kwa bao 1-0.

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 41(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha ikiwa ni moja ya kanuni ambazo zinaongoza ligi kuu inayodhaminiwa na Vodacom.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka