Connect with us

Soka

Bodi Ya ligi Yamshukia Zahera

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amepigwa faini ya shilingi laki tano baada ya kuvaa mavazi yasiyo nadhifu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu shooting ambapo timu hiyo ilipoteza kwa bao moja.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji ligi kuu namba 14(2m) inayohusu taratibu za mchezo.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya kamati ya bodi ya ligi kuu ya uendeshaji na usimamizi wa ligi kukaa kikao septemba 2 ili kupitia matukio mbalimbali ya ligi kuu iliyoanza agosti 24.

Pia klabu ya Yanga nayo imepewa onyo kwa kushindwa kusimamia kocha huyo kuhakikisha anavaa mavazi nadhifu akiwa kama kiongozi wa benchi la ufundi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka