Connect with us

Soka

Bale Aikoa R/Madrid

Jiwe walilolikataa waashi limekua jiwe kuu baada ya jana Gareth Bale kuisawazishia Real Madrid na kufanya iondoke na pointi moja ugenini dhidi ya Villarreal katika sare ya mabao 2-2 ugenini katika uwanja wa Estadio da ceramica.

Gerrad Moreno alipata bao dakika ya 12 baada ya makosa ya Sergio Ramos na kuwafanya wenyeji kutangulia baada ya bao hilo kuthibitishwa na mwamuzi wa video(VAR) licha ya juhudi za kipa Thibaus Courtois kuokoa mpira huo.

Licha ya Karim Benzema kugongesha mwamba,alikua ni Gareth bale aliyeisawazishia madrid baada ya kazi nzuri ya pamoja ya Dan Calvajar na Luka Jovic na kuwapita mabeki wa Villarreal na kumrahisishia kazi Bale ambaye alimalizia kazi nzuri.

Moi Gomez aliipatia Villarreal bao la pili baada ya kipa Thibaus Courtois kupangua mpira ndani ya boxi na kumfanya mfungaji kupata kazi rahisi akimalia shuti hilo lililopigwa na Gerrad Moreno.

Dakika ya 86 bale aliipatia Madrid bao la kusawazisha baada ya kupiga mpira uliomshinda kipa wa Villarreal na kufanya ubao kusomeka 2-2 na kipindi cha dakika ya nyongeza winga huyo alitolewa baada ya kupata kadi mbili za njano.

Winga huyo hivi sasa amefikisha mabao matatu katika mechi mbili na kuzua swali kwa mashabiki kuhusu msitakabari wa staa huyo baada ya kocha kumtaka staa huyo kufungasha vilago klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka