Connect with us

Soka

Manungu,Mabatini Vyapigwa Kufuri

Bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara (TPLB) imevifungia viwanja vya Mwadui complex,Manungu na Mabitini kutumika katika mechi za ligi  kuu mpaka hapo vitakapofanyiwa ukarabati na kuthibitishwa na bodi hiyo kuwa vinafaa kutumika.

Akizungumza na waandishi wa habari afisa mtendaji mkuu wa bodi hiyo Michael Wambura amesema viwanja hivyo havirithishi kutumika katika michezo ya ligi kuu kutokana na kukosa ubora unaotakiwa yakiwemo majakwaa ya mashabiki.

Uwanja wa mabatini unatumiwa na klabu ya Jkt Tanzania kama uwanja wa nyumbani huku ule wa Manungu unatumiwa na Mtibwa Sugar na ule wa Mwadui Complex ulioko shinyanga unatumiwa na timu ya Mwadui Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka