Connect with us

Soka

Ninja Atua kwa Kadabra

Beki wa zamani wa Yanga Abdalah Shaibu “Ninja” amefanikiwa kujiunga na timu ya L.A Galaxy anayoichezea staa Zlatan Ibrahimovich ambayo inashiriki ligi kuu ya nchini Marekani.

Ninja amesajiliwa na MFK Kalvina ya ligi daraja la tatu nchini Czech ambayo amesaini mkataba wa miaka minne kama mchezaji huru na ametolewa kwa mkopo wa mwaka mmoja katika klabu hiyo ya Galaxy inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani ya MLS.

Awali beki huyo alisajiliwa na Yanga akitokea Mlandege ya Zanzibar na baada ya msimu mmoja wa changamoto alijizolea sifa kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na kujituma na nidhamu ya mchezo aliyokua nayo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka