Connect with us

Soka

Himid Mao Wa Kimataifa

Kiungo wa zamani wa Azam Fc Himid Mao Mkami amejiunga rasmi na timu ya ENPPI akitokea klabu ya Petrojet ya huko huko nchini Misri.

Mao mtoto wa kiungo wa zamani wa timu ya taifa Mao Mkami amejiunga na timu hiyo aliyokua akiichezea mtanzania mwingine Shiza Kichuya baada ya timu yake ya awali ya Petrojet kushuka daraja.

Mao ameichezea taifa stars toka ngazi ya vijana mpaka ya wakubwa na amefanikisha kuisaidia kushiriki michuano ya mataifa ya Africa(Afcon 2019) nchini Misri licha ya timu hiyo kutolewa katika hatua za awali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka