Connect with us

Makala

Stars ya Chan Yatangazwa

Kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) Etienne Ndayiragije ametangaza kikosi cha wachezaji 25 watakaounda timu kwa ajili ya mchezo wa awali wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) kitakachoingia kambini mwezi julai kujiandaa na mechi dhidi ya Kenya.

Kocha huyu Mrundi anayesaidiwa na mtanzania Seleman Matola ametaja kikosi hicho huku akiwatema baadhi ya wachezaji waliokuwamo katika kikosi kilichokwenda nchini Misri katika michuano ya Afcon.Wachezaji waliotemwa ni Mohamed Hussein,Agrey Moriss,Ally Sonso na wengine huku akiwarejesha kikosini Jonas Mkude,Ibrahim Ajibu na kinda wa Yanga Paul Godfrey Boxer.

Kikosi kamili ni makipa Aishi Manula,Juma Kaseja na Metacha Mnata.Mabeki ni Paul Godfrey,Kelvin Yondani,Erasto Nyoni,Boniface Maganga,Gadiel Michael,Paul Ngarema,David Mwantika,Idd Mwobi huku Viungo wakiwa ni Jonas Mkude,Abdalaziz Makame,Mudathir Yahaya,Ibrahim Ajibu,Salum Abubakar,Feisal salum,Frank Domayo,Hassan Dilunga,Idd Nado na washambualiaji ni John Boko,Salim Aiyee,Shaban Idd Chilunda,Masoud Abdalah.

Taifa stars inayodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti itaingia kambini julai 21 jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala