Connect with us

Soka

Kotei Aingia Rada za Yanga

Baada ya kusikia James Kotei ana nafasi kubwa ya kutopewa mkataba na Simba sc baadhi ya viongozi wa Yanga sc wameanza kummendea mchezaji huyo ili aweze kuichezea timu hiyo mwakani.

Viongozi hao tayari wanadaiwa kuanza kumshawishi kocha Mwinyi Zahera kuona kama atakubaliana na usajili wa mchezaji huyo kiraka anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi pamoja na ile ya kiungo hasa mkabaji.

Kotei amemaliza mkataba na Simba sc na mpaka sasa hakuna mazungumzo yeyote yaliyofanyika kuhusu kuongeza mkataba mpya kwa kiraka huyo ambaye yupo kwao nchini ghana akisikilizia kama atapigiwa simu na viongozi hao wa simba.

Yanga walikua na nia ya kumsajili kotei miaka miwili iliyopita japo dili hilo halikufanikiwa baada ya baadhi ya viongozi wa simba kumuwahi na kumsainisha mkataba kiungo huyo mpole anayetimiza majukumu yake vyema uwanjani.

Ili dili hilo liweze kukamilika ni lazima kocha Mwinyi Zahera apitishe usajili wa mchezaji huyo ambaye pia taarifa zinadai anaweza kujiunga na Kaizer chiefs za nchini Afrika ya Kusini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka