Connect with us

Soka

Mwantika Arejeshwa Stars

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) Emmanuel Amunike amemuita kikosini beki wa Azam Fc David Mwantika kwenda kuchukua nafasi ya mchezaji mwenzake wa klabu hiyo Aggrey Morris Ambrose katika kambi ya timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya Afcon.

Taarifa zinasema Amunike amechukua maamuzi hayo baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya afya ya Aggrey ambaye aliumia katika mechi ya kupasha moto misuli dhidi ya Misri,hivyo mabadiliko hayo ya mwishoni yamechukuliwa ili kumpa nafasi beki huyo apone vizuri.

Morris aliumia katika mchezo katika dakika ya 74 na nafasi yake ilichukuliwa na Ally Mtoni Sonso japo Tanzania ililala kwa goli moja liilofungwa na Ahmed Elmohamady dakika ya 64 kwa kichwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka