Connect with us

Soka

Yanga Kushiriki Klabu Bingwa Afrika

Timu ya Yanga imepata bahati ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwakani baada ya kumaliza nafasi ya pili ya ligi kuu bara.Timu hiyo itaungana na Simba katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika huku Azam itaungana na Kmc kushiriki kombe la kombe la shirikisho.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini(Tff) imeonyesha kuwa Tanzania imepata nafasi ya kuingiza timu nne katika mashindano yanayoandaliwa na shrikisho la soka barani Afrika (Caf) baada ya kupanda kwa viwango vya ubora mpaka nafasi ya 12 baada ya vilabu vya Simba na Yanga kufanya vizuri katika michuano hiyo miaka ya karibuni.

Azam itaungana na Kmc kushiriki kombe la shirikisho kwa mujibu wa kanuni za Tff ambapo Azam ni mshindi wa michuano ya kombe la shirikisho nchini hivyo anajikatia tiketi ya michuano hiyo huku Kmc wakiingia kama washindi wa nafasi ya nne ya ligi kuu bara.

Tff wamepokea barua kutoka Caf kuwajulisha kuhusu ushiriki wa timu hizo hivyo usajili upo wazi mpaka june 30 mwaka huu ili kukamilisha usajili wa kuingiza timu hizo.Pia Tff imezitaka klabu hizo kukamilisha usajili kufikia mfumo wa kimtandao wa CMS.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka