Connect with us

Makala

Sanga Alia na Maslahi ya Wachezaji Npl

Mheshimiwa mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga ameendelea kulilia maendeleo ya mpira wa miguu nchini ambapo amelalamikia maslahi madogo ya wachezaji wa soka nchini hasa wale wanaocheza ligi kuu na ligi daraja la kwanza nchini.

Mheshimiwa mbunge ameyasema hayo alipokua akichangia katika bajeti ya Wizara ya Michezo na Utamaduni iliyosomwa hivi leo na Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ambaye ni Waziri wa Wizara hiyo.

Katika bejeti hiyo licha ya Serikali kutenga takribani bilioni 10 kukarabati viwanja vya soka nchini vilivyo chini ya Chama cha Mapinduzi jambo ambalo pia halikumzuia Mheshimwa Sanga kuchangia kuhusu umuhimu wa kuboreshwa kwa maslahi ya wachezaji mpira nchini.

“Vijana wetu wa ligi zote kuanzia ligi kuu wamekua wakifanya kazi ya jasho na damu lakini wana maslahi madogo sana hivyo napendekeza serikali kuweka kiwango cha chini cha mshahara kiwe Milioni moja..”alisema mheshimiwa Sanga.

Wizara ya Michezo na utamaduni nchini imewasilisha bajeti hiyo mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano nchini ambapo Viongozi wote wa Wizara hiyo walihudhuria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala