Connect with us

Makala

Messi huyoo PSG

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi amekubali mkataba wa miaka miwili kujiunga na matajiri wa jiji la Paris PSG hadi mwaka 2023 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Messi ataweka kibindoni kiasi cha Euro milioni 35 kama mshahara na marupurupu kukipiga Parc De Prince.

Mshambuliaji wa Kibrazil Neymar ambaye ni rafiki mkubwa wa Messi amekuwa akisukuma sana dili hilo.PSG ni klabu pekee iliyowasiliana na Messi moja kwa moja tangu alhamisi klabu ya Barcelona ilipotangaza kuwa ataondoka Nou Camp na anatarjiwa kutangazwa rasmi kama mchezaji wa PSG ndani ya masaa machache yajayo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala