Connect with us

Soka

Manula Basi Tena Simba Sc

Golikipa wa Simba sc na Timu ya Taifa ya Tanzania Aishi Manula ataikosa michezo miwili ya robo fainali ya Klabu yake ya Simba dhidi ya Al Ahly kutokana na kupata majeraha akiwa na Timu ya Taifa ilipokua ikicheza na Bulgaria nchini Azerbaijan.

Manula aliumia kipindi cha kwanza katika mchezo huo na taarifa zinaeleza kuwa Manula ametonesha jeraha lake ambalo alilipata kipindi cha nyuma hali iliyopelekea kufanya upasuaji ambao ulimlazimu kukaa nje Kwa miezi kadhaa.

Kwa mujibu wa meneja wa mchezaji huyo Jemedari Said  amesema kuwa jeraha hilo litamfanya sasa kukaa nje ya Uwanja Kwa muda mrefu zaidi ili kuhakikisha anapona kabisa na kukaa sawa ndipo anaweza kuanza tena kucheza mechi za ushindani.

Simba sc siku ya Jumamosi ijumaa itakua na mchezo mgumu dhidi ya Al Ahly ambapo sasa ni wazi golini atakaa kipa Ayoub Lakred huku Ally Salim atakaa kama kipa wa akiba ambapo pia anaweza kukaa kipa Hussein Abel.

Manula tangu arejeaa kutoka katika majeraha hayo hajaweza kurudisha kiwango chake cha awali ambapo amekua akifunga mabao rahisi tofauti na awali ikiwemo kipigo cha 5-1 kutoka kwa Yanga sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka