Connect with us

Soka

Simba Sc Watua kwa Beki Coastal Union

Uongozi wa klab ya Simba Umefufua mpango wa kuipata saini ya mlinzi wa kati wa klabu ya Coastal Union Lameck Elias Lawi kuja kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo kusaidiana na Henock Inonga na Che Fondoh Malone.

Imefahamika kuwa ofa kutoka Simba Sc kwenda kwa wagosi wa kaya tayari imeshatumwa na kinachosubiriwa sasa ni majibu na makubaliano mengine ya kimkataba baina ya klabu hiyo pamoja na mchezaji mwenyewe.

Lawi ambaye ni beki bora chipukizi nchini kwa msimu uliopita ameonyesha nia ya kujiunga na Simba sc ambapo kutokana na kuwa na mkataba na Coastal hana budi kusubiri makubaliano baina ya klabu hizo yakamilike ndipo ajiunge na wekundi hao wa msimbazi.

Simba sc ipo katika mpango kabambe wa kufanya maboresho makubwa katika kikosi chake ambacho kinasuasua kutokana na mastaa wa timu hiyo asilimia kubwa kuonekana kuchoka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka