Connect with us

Soka

Ni Bruno Fernandes Tena

Kiungo sukari wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes ameibuka mchezaji bora wa mwezi juni kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwa na msimu mzuri klabuni hapo.

Bruno aliyechangia jumla ya mabao 13 klabuni hapo msimu huu ametwaa tuzo hiyo baada ya kufanya vizuri tangu ligi irejee kutoka katika janga la Corona mwezi uliopita ambapo amefanikiwa kufunga mabao matatu kwa mwezi juni.

Bruno anakuwa mchezaji wa pili wa klabu ya Manchester United kushinda tuzo hiyo mfululizo tangu aliposhinda Cristiano Ronaldo mwaka 2006.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka