Connect with us

Makala

Lusajo Awapiku Aziz Ki,Feisal

Mshambuliaji wa klabu ya Mashujaa Fc Reliants Lusajo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Mei akiwapiku mastaa Stephane Aziz Ki wa klabu ya Yanga sc na Feisal Salum wa klabu ya Azam Fc kutokana na mabao yake kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa timu yake ya Mashujaa Fc.

Kwa mujibu wa kamati ya tuzo hizo za ligi kuu ni kwamba Mashujaa ilikua na hatihati ya kushuka daraja lakini mabao matano ya Lusajo sambamba na asisti zake mbili yalisaidia kuipa ushindi timu hiyo katika michezo minne kati ya sita na kuisaidia timu kupanda mpaka nafasi ya nane ya msimamo na kuiepusha na dhahama ya kushuka daraja tofauti na mabao ya Ki na Feisal.

Azizi Ki alifunga jumla ya mabao sita akiongoza Yanga sc kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Nbc kwa mara ya tatu mfululizo huku Feisal nae akiisadia timu yake kumaliza nafasi ya pili na kuipa tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika lakini michango ya mastaa hao haikutosha kuwapa tuzo hiyo.

Tuzo za mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu na kocha bora wa mwezi hutolewa na bodi ya ligi kupitia kamati maalumu ya kufanya tathmini ya mwenendo wa ligi kuu nchini ambao pia hupiga kura ya mchezaji bora wa mwezi kwa wachezaji na makocha watatu wenye mchango mkubwa kwa timu zao kwa mwezi husika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala