Connect with us

Soka

Mo salah na Mkataba Liverpool

Mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah anasema klabu yake bado haijazungumzia mkataba wake mpya ambao unafika tamati msimu wa 2023.

Mo Salah anasema “hakuna mtu yoyote kutoka Liverpool ambaye amemwendea kwa ajili ya kujadili uwezekano wa kusaini kandarasi mpya klabuni hapo”

Mkataba wa sasa wa Salah huko Liverpool unaendelea hadi msimu wa joto wa 2023 huku akivuta kiasi cha mshahara wa Paundi laki mbili kwa wiki.

Lakini mshambuliaji huyo wa Misri anasema kwa sasa hakuna matarajio ya kuongezwa mkataba mpya baada ya mabosi wake kuuchuna huku Real Madrid,Psg na Juventus wakimtazama kwa matamanio makubwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka