Connect with us

Makala

Yanga sc Yawasili Arusha

Msafara wa mastaa wa klabu ya Yanga sc umefanikiwa kuwasili salama jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Coastal Union unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini humo.

Yanga sc imewasili ikiwa na zaidi ya asilimia kubwa ya mastaa wake ambao wameonekana uwanja wa ndege wakiwasili kwa ajili ya mchezo huo huku kipa Djigui Diarra akikosekana katika msafara huo huku haijajulikana sababu kuu ya kukosekana huko.

Yanga sc itakua na kibarua kigumu kuchukua alama tatu mbele ya Coastal Union ambayo wiki hii imemtambulisha kocha Juma Mwambusi kama kocha mkuu klabuni hapo.

Ikiwa inawania ubingwa wa ligi kuu nchini Yanga sc mpaka sasa imeshinda michezo yote sita iliyocheza ya ligi kuu ikisusanya alama 18 huku Coastal Union ikiwa na alama nane baada ya kucheza michezo nane ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala