Lamine Aipaisha Yanga Moro

0

Yanga Sc imefanikiwa kusepa na pointi tatu leo katka uwanja wa Jamuhuri uliopo jijini Morogoro baada ya kuwapa kichapo cha bao 1-0 Mtibwa Sugar kupitia kiungo wao mpya Lamine Moro.

Lamine alipachika bao la ushindi dakika ya 61 kupitia kona iliyopgwa na Carlos Carlinhos na kuibua shangwe kwa mashabiki baada ya bao hilo kudumu hadi dakika 90 za mchezo zilipokamilika.

Mechi ya leo inakamilisha mzunguko wa nne wa ligi kuu japo haukuwa mpira wa kiufundi kutokana na uwanja kutokuwa mzuri.

Leave A Reply

Your email address will not be published.