Connect with us

Makala

Tabora United Yainyuka Pamba Jiji

Hali imekua tete kwa klabu ya Pamba Jiji baada ya jioni ya leo kukubali kipigo cha 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Bao pekee la Ogochukwu Morice dakika ya 77 kwa penati liliimaliza Pamba Jiji ambao sasa imefikisha michezo tisa bila kuonja ushindi wowote katika ligi kuu nchini.

Ushindi huo unakua wa tatu kwa Tabora United msimu huu na sasa imefikisha alama 11 ikicheza michezo 9 ya ligi kuu nchini na kupanda mpaka nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu nchini.

Pamba Jiji yenyewe mpaka sasa pamoja na kucheza michezo 9 ya ligi kuu haijapata ushindi wowote ikiwa nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na alama 5 pekee katika michezo 9 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala