Connect with us

Makala

Yanga sc,Kibwana Fresh

Ikiwa amebakiza muda usiozidi miezi miwili  kumaliza mkataba wake katika klabu ya Yanga sc,Beki Kibwana Shomari inasemekana amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kusalia klabuni hapo baada ya mazungumzo baina ya pande mbili kwenda sawa.

Mwakilishi wa mchezaji huyo amekutana na viongozi wa Yanga sc na kuzungumza kuhusu dili hilo la kuongeza mkataba mpya klabu hapo ambapo kwa zaidi ya asilimia tisini wamekubaliana kimsingi na imebaki kusaini mkataba mpya wa beki huyo kusalia jangwani.

Yanga sc ilimsajili Kibwana misimu msimu 2020/2021 akitokea Mtibwa Sugar baada ya kununua mkataba wake na amekua moja ya nguzo ya timu hiyo katika upande wa ulinzi wa kulia ama kushoto kutokana na mahitaji ya Mwalimu Nasreddine Nabi.

Mchezaji huyo ameendelea kung’ara licha ya ujio wa Djuma Shabani katika upande wa kulia japo hakua na msimu mzuri baada ya kuwa nje ya uwanja kwa juda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala