Connect with us

Makala

Aucho Mbioni Kuivaa Simba sc

Kiungo Khalid Aucho ambaye alikua na majeruhi kwa wiki kadhaa tayari amerejea kikosini Yanga sc ambapo ameonekana akifanya mazoezi na wenzake baada ya kumaliza programu ya utimamu wa mwili.

Kiungo huyo kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Yanga sc aliumia  katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar jeraha ambalo lilipona lakini alijitonesha katika mazoezi ya timu ya Taifa ya Uganda alikoitwa wiki chache zilizopita katika michezo ya kimataifa.

Aucho anakuja kuongeza ubora wa safu ya kiungo ya Yanga sc ambayo ilipwaya kutokana na kuumia kwake pamoja na kiungo Feisal Salum hivyo kufanya kikosi kuwa na viungo wa asili wa eneo la kati wawili pekee ambao ni Zawadi Mauya na Salum Abubakari ‘Sure Boy’.

Kocha Nabi sasa atakua anafurahia kurejea kwa Aucho kutokana na michezo migumu iliyo mbele yake dhidi ya Namungo Fc na Simba sc ambayo itapisha wiki pekee huku michezo hiyo ikibeba picha halisi ya safari ya ubingwa ya klabu hiyo ambao iliukosa kwa takribani miaka minne mfululizo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala