Friday, May 9, 2025
Home Makala Simba sc Wamtambulisha Straike la Tp Mazembe

Simba sc Wamtambulisha Straike la Tp Mazembe

by Sports Leo
0 comments

Jean Baleke ametambulishwa kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Simba sc kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja baada ya timu hizo mbili kufikia makubaliano huku kukiwa na kipengele cha kuongeza zaidi muda huo kwa mchezaji huyo.

Baleke mwenye miaka 21 amejiunga na klabu ya Simba sc akitokea nchini Lebanon alipokua anacheza katika klabu ya Nejmeh SC ya nchini humo na baada ya mkopo huyo kuisha alilazimika kurudi Tp Mazembe na kisha akapata dili hilo la kujiunga na Simba sc.

Baleke aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu nchini Congo msimu wa 2020/2021 akiwa na timu ya JS Kinshasa alipofunga jumla ya  magoli 14 na akafanikiwa kusajiliwa na Tp Mazembe msimu uliofuatia lakini kiwango chake hakikuwaridhisha mabosi hao na kuamua kumtoa kwa mkopo.

banner

Simba sc imefanikiwa kumsajili staa huyo kuja kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji lililokua chini ya Moses Phiri na Cletous Chama ambapo sasa kutakua na machaguo mbalimbali eneo hilo la ushambuliaji.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.