Thursday, May 8, 2025
Home Makala Msuva Atua Uarabuni

Msuva Atua Uarabuni

by Sports Leo
0 comments

Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Wydad Casablanca Simon Msuva amejiunga na klabu ya Alqadsiah inayoshiriki ligi daraja la pili nchini  Saudi Arabia ambapo amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine zaidi.

Winga huyo hakua na timu kwa muda mrefu kutokana na kuwa na mgogoro kuhusu fedha za usajili na mishahara na klabu hiyo ya Wydad ambayo ilimsajili kutoka Difaa El Jadid ya huko huko nchini Morroco kiasi cha kesi kufika katika Shirikisho la soka Duniani (Fifa) ambao waliamuru klabu hiyo kumlipa mchezaji huyo kiasi cha Bilioni 1.6 ikiwemo pamoja na fidia.

Usajili huo unahitimisha tetesi za awali kuwa anaweza kusalia nchini Tanzania kujiunga na klabu yake ya zamani ya Yanga sc huku pia alikua akihusishwa kujiunga na Simba sc.

banner

Msuva atajumuika na mchezaji wa zamani wa Nkana Fc ya Zambia na Al ahly Sc Walter Bwallya katika klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humu huku ikisemekana atalipwa kiasi kikubwa cha mshahara kwa wiki.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.