Connect with us

Makala

Sopu Ailaza Somalia

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Coastal Union ambaye kwa sasa amejiunga na klabu ya Azam Fc Abdul Sopu ameihakikishia alama tatu timu ya taifa ya Tanzania katika mchezo wa awali kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ya nchi(Chan) dhidi ya Somalia.

Sopu alifunga bao hilo dakika ya 47 ya mchezo akiunganisha krosi ya Kibwana Shomari kwa kichwa na kuifanya Stars kuhitaji sare yeyote ama ushindi katika mchezo wa marudiano ili iweze kwenda hatua inayofuata.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika  suluhu huku Stars wakikosa nafasi za kufunga kupitia kwa Kibu Dennis na Feisal Salum.

Mshindi katika raundi hii anatarajiwa kumenyana na Uganda ili kupata mwakilishi katika michuano hiyo kwa upande wa Afrika Mashariki na kati.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala