Thursday, May 8, 2025
Home Makala Azam Fc Yatua kwa Mshery

Azam Fc Yatua kwa Mshery

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imewasiliana na uongozi wa Kipa AbouTwalib Mshery ili kumsajili baada ya kushindwa kumbakisha kipa Mustapha Mohamed aliyeko kwa mkopo kutokea klabu ya El Merrekh Fc ya Sudan.

Azam Fc inamuona Mshery kama chaguo sahihi katika mradi wao wa kuboresha kikosi Chao cha muda mrefu ambapo sambamba na mshahara mnono pia wamemuahidi kumpa muda wa kucheza mara kwa mara tofauti na klabuni kwake Yanga sc.

Tayari ofa hiyo imeshapokelewa na uongozi wa mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Yanga sc unafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu japo tayari klabu imeonyesha nia ya kumuongezea.

banner

Yanga sc baada ya Djigui Diarra inamuona Mshery ni mbadala sahihi wa muda mrefu klabuno hapo na ikizingatiwa making hao wote wanamaliza mikataba yao mwezi huu.

Azam Fc inamshawishi Mustapha kuomba kuondoka El Merrekh baada ya klabu hiyo kumhitaji kwa ajili ya msimu ujao.

El Merrekh iliwatoa mastaa wake wengi kwa mkopo katika vilabu kadhaa kutokana na ligi kuu nchini Sudan kusimama kutokana na machafuko ya kisiasa hivyo kuhitaji kulinda viwango vya mastaa hao.

Mbali na Mustapha na Mshery pia klabu hiyo inavutuwa kumrejesha Aishi Manula lakini kipa huyo anahitaji muda zaidi aweze kupona baada ya kuumia na kuwa nje kwa muda mrefu zaidi.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.