Home Soka Yanga yatinga nusu fainali Mapinduzi

Yanga yatinga nusu fainali Mapinduzi

by Sports Leo
0 comments

Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Yanga sc wamefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya kombe hilo licha ya kulazimishwa sare ya 2-2 na mabingwa wa soka Zanzibar KMKM leo hii.

Yanga ikiwa na maingizo mawili mapya katika kikosi kilichoshinda mchezo wa kwanza walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa 1-0 goli likifungwa na mshambuliaji Heritier Makambo dakika ya 45 kwa kichwa.

Kipindi cha pili KMKM walijitahidi kufanya mashambulizi ya hapa na pale na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Abraham Ali dakika ya 54 akitumia vema mpira wa adhabu uliopigwa na mchezaji wa zamani wa Yanga Mwinyi Haji.

banner

Baada ya goli hilo Yanga walifananya mabadiliko ya kuwaingiza Moloko,Farid na David Bryson kuongeza nguvu ya kushambulia na hatimaye Fei Toto kuwapa bao la pili kwa mkwaju mkali dakika ya 80.Zikiwa zimebaki dakika mbili za nyongeza mpira kumalizika KMKM walichomoa na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Hata hivyo kwa matokeo hayo mabingwa hao watetezi wamekata tiketi kwa kumaliza wa kwanza kwenye kundi B.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited