Connect with us

Makala

Yanga Sc Watua Zanzibar Mapema

Msafara wa kikosi cha timu ya Yanga sc tayari kimewasili mjini Unguja Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa pili wa marudiano hatua ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika utakaofanyika katika uwanja wa Amaani Visiwani humo siku ya Jumamosi Septemba 21 dhidi ya Cbe SA ya nchini Ethiopia.

Katika mchezo wa awali uliofanyika nchini Ethiopia katika uwanja wa Abebe Bikila,Yanga sc ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Prince Dube dakika ya 25.

Ikiingia na mtaji huo wa bao moja,Mashabiki wa klabu hiyo mpaka sasa wanaamini kuwa wataibuka na ushindi wa kishindo na kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Tayari Uongozi wa klabu hiyo umeingia mkataba ya udhamini wa mchezo huo na makampuni na Taasisi ikiwemo Bodi ya Utalii Zanzibar ambao wamesaidia baadhi ya maandalizi kwa klabu hiyo.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru sana Wadhamini ambao wamejitokeza kufanya kazi na sisi. Kuelekea mechi yetu dhidi ya CBE tayari tumeshakusanya zaidi ya Milion 200 nje ya mauzo ya tiketi. Asanteni sana wadhamini wetu” Alisema mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Ali Kamwe wakati akizungumza na waandishi wa habari visiwani humo.

“Jumamosi ni siku ya kwenda kufyeka kichaka cha kujifanya wao ni bora kuliko sisi kwneye rank za CAF. Haiwezekani timu tumeifunga goli 7 inakaa juu yetu sisi kwenye rank za CAF. Kila Mwanayanga anapaswa kuhakikisha hii ni jumamosi ya kuhakikisha tunakwenda kukaa juu.”alimalizia kusema Ally Kamwe

Msimu huu ikiwa chini ya kocha Miguel Gamondi klabu hiyo inaamini kuwa itafika walau hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Msimu uliopita Yanga sc ilitolewa na Mamelod Sundowns katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala