Thursday, May 8, 2025
Home Makala Singida Black Stars Kileleni Nbc

Singida Black Stars Kileleni Nbc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Singida Black Stars imeendelea kung’angania kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ccm Liti mjini Singida.

Black Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba sc Patrick Aussems ilifanikiwa kupata mabao yake yakifungwa na Marouf Tchakei dakika za 56 kwa shuti kali akipokea pasi kutoka kwa Emmanuel Keyeke na 89 kwa penati kufuatia Beki wa Namungo Fc kumfanyia madhambi mshambuliaji Yonta Camara ndani ya eneo la 18 na mwamuzi kuamuru penati.

Black Stars sasa baada ya kupata alama tatu moja kwa moja wamekaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini wakiwa na alama 19 wakicheza michezo saba huku Namungo Fc wakiwa nafasi ya 13 na alama 6 wakicheza michezo saba ya ligi kuu.

banner

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.