Home Makala Ronaldo Akumbwa na Virusi

Ronaldo Akumbwa na Virusi

by Sports Leo
0 comments

Mchezaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Al-nassr Fc Cristiano Ronaldo amepatikana na maambukizi ya Virusi ambavyo madaktari wa klabu ya Al-nassr FC hawakutaja ni virusi vya aina gani.

Madaktari wa klabu wanasema wamesema kuwa staa huyo ana virusi mwilini hivyo hatoweza kucheza mchezo wowote klabuni hapo.

“Cristiano Ronaldo ana virusi jambo ambalo limemsababisha kushindwa kusafiri Jana Jumatatu, kuelekea Iraq kucheza mchezo dhidi ya A-Shorta FC katika michuano ya AFC champions League Elite”.Alisema moja ya madaktari wa klabu hiyo.

banner

Taarifa ya klabu ya Al-nassr Fc imeeleza kuwa staa huyo hakua anajisikia vizuri hivyo kulazimika kufanyiwa vipimo zaidi.

“Cristiano Ronaldo hakuwa anajiskia vizuri kiafya na baadae alitambulika kuwa na maambukizi ya virusi na wataalamu wa afya wa klabu yetu walitambua hilo, hivyo Ronaldo anatakiwa apumzike na kupata matibabu mpaka atakapokua sawa”.

Ronaldo amefanikiwa kuleta hamasa ya kutosha nchini humo kuhusu mchezo wa soka baada ya kusajiliwa na klabu hiyo ya barani Asia

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.