Connect with us

Soka

Ramadhan Yasimamisha Ligi Z’bar

Ligi kuu ya soka Visiwani Zanzibar inatarajiwa kusimama kwa kipindi cha mwezi mmoja ili kupisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na bodi inayosimamia ligi hiyo.

Ligi hiyo inasimama sambamba na ligi daraja la kwanza na ligi ya mkoa baada ya kumalizika kwa mzunguko wa ishirini wa ligi hiyo ambapo pia bodi hiyo imepangua ratiba za baadhi ya michezo ya ligi hiyo kuanzia mwezi wa tatu.

Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi, michezo hiyo ni timu ya Hard Rock dhidi ya Kipanga FC ambao ulitakiwa kuchezwa Februari 29, lakini ulichezwa jana Jumanne Februari 27 katika Uwanja wa FFU Finya – Pemba.

Pia mchezo kati ya timu ya Mafunzo FC dhidi ya JKU SC sasa utachezwa Jumapili ijayo, Machi 3 lakini awali ulitakiwa kupigwa Ijumaa, Machi Mosi huku mtanange kati ya Uhamiaji FC dhidi ya Jamhuri FC uliotakiwa kuchezwa Machi Machi 3 hivi sasa utapingwa Machi Mosi.

Kwa mujibu wa mabadiliko michezo mingine itachezwa kama ilivyopangwa ambapo mabingwa KMKM SC itacheza na Ngome FC katika Uwanja wa Mao A, huku Malindi dhidi ya Maendeleo United utachezwa katika uwanja wa Mao B Februari 29.

Majirani Dabi itachezwa Machi 2 kati ya Mlandenge dhidi ya Kundemba ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Mao A na Zimamoto dhidi ya KVZ wataminyana Machi 3.

Mbali na kusimama kwa Ligi Kuu Zanzibar, pia imezoeleka kila msimu wa mfungo wa Ramadhani, Ligi zingine pia husimamishwa ambapo kwa sasa ni ligi kuu,ligi daraja la kwanza sambamba na ligi ya mkoa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka