Home Soka PSG Mabingwa Ligue 1

PSG Mabingwa Ligue 1

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya PSG imetagazwa mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1 baada ya serikali kuamua kufuta michezo yote kwa mwaka huu kutokana na janga la ugonjwa wa covid-19.

Awali serikali ya Ufaransa ilitangaza kusimamisha michezo yote nchini humo hadi mwezi mei tarehe 11 ambapo shirikisho la soka nchini humo lilitangaza mpango wa kuanza mechi za ligi mwezi wa sita kabla ya serikali kubadilisha uamuzi huo siku ya jumanne baada ya waziri mkuu wa nchini hiyo Edouard Phillipe kutangaza kuwa michezo itarudi mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Kwa maana hiyo timu za PSG, Marseille, na Rennes watashiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya (champions league) kwa msimu wa 2020/21 huku timu za Lille, Reims, na Nice watashiriki Europa League msimu wa 2020/21 .

banner

Wakati huo huo Amiens na Toulouse zimeshuka kutoka Ligue 1 wakati timu za Lorient na Lens zimepanda Ligue 1 .

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited