Klabu ya Yanga sc imeinia matatani kufuatia sakata la usajili wa Kipa Aboutwalib Mshery ambapo klabu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar imelalamika katika vyombo vya habari kutolipwa ada ya usajili kama walivyokubaliana wakati wa usajili.
Thobias Kifaru ambaye ni msemaji wa klabu hiyo amesema kuwa makubaliano yalikua mazuri huku wao kama timu wakiaamini Yanga sc watafanya malipo hayo mapema.
“Yalifanyika makubaliano ya pande mbili tukiamini Yanga ni watu wazima na watatelekeza mkataba unavyosema, lakini mpaka sasa hakuna hata moja lililofanyika lakini Tangu January mpaka sasa hatujaona kitu”.
”Mbaya zaidi Mawasiliano yetu na wao sio mazuri na hatukutaka haya mambo yafike kwenye Vyombo vya Habari, lakini kinachofanyika sasa ni sisi kuwafuata wao, lakini ilitakiwa wao watufuate sisi,Hii ni kama tunawambeleza juu ya malipo ya Abuutwalib Mshery”.
“Tunaendelea kuwasubiri na tutakuwa wapole, lakini hawajafanya vile ambavyo tulitarajia.
“Mtibwa Sugar tumetoa vijana wengi kwenda Yanga, kikubwa watazame makubaliano yetu na wao yanasemaje”.
Yanga sc ilimsajili Mshery ili awe mbadala wa Djigui Diarra ambaye alikwenda kwenye michuano ya Afcon nchini Cameroon na kusababisha klabu hiyo kubakia na kipa mmoja Erick Johora hivyo kumsajili Mshery.