Home Soka Corona Yampa Tuzo Rashford

Corona Yampa Tuzo Rashford

by Sports Leo
0 comments

Nyota wa Manchester United Marcus Rashford ametambuliwa kwa kupewa tuzo kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19 na ofisi ya Sheriff ya huko katika jiji la Manchester.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United amekuwa akifanya kazi na moja ya mashirika makubwa ya Uingereza, kutoa msaada kwa watoto wakati wa janga la Covid-19 .

Staa huyo alisaidia kuchangisha kiasi cha paundi milioni 20 katika oganaizesheni ya Fareshare ili kupambana na baa la njaa na ukosefu wa chakula kufuatia janga la Corona ambapo takribani watoto milioni 2.8 walikua katika hatari ya kukosa chakula hasa baada ya shule kufungwa mwezi machi mwaka huu.

banner

Juhudi zilitambuliwa na Sherifu huyo wa jiji hilo Eamonn O’Neal ambaye alimtumia kadi maalumu ya pongezi ambapo Rashford alionekana kufurahishwa na pongezi hizo baada ya kuziweka wazi kupitia mtandao wake wa Twiter.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited