Connect with us

Soka

Kocha Awapa Kiwewe Kenya

Timu ya taifa ya Kenya(Harambee Stars) sasa watashiriki mchujo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar baada ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kuafikiana na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuhusu jinsi ambavyo zaidi ya bilioni 2.4 zinazodaiwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Adel Amrouche, zitalipwa .

Awali, FIFA ilitarajiwa kuelekeza fedha za maendeleo ya soka ambazo Kenya ambazo wanachama wote wa FIFA hupewa kila mwaka kutumika kumlipa kocha huyo Amrouche, kocha mzawa wa Ubelgiji na raia wa Algeria ambaye kwa sasa anaifundisha  timu ya taifa ya Botswana.

Awali iliamliwa na mahakama ya juu ya michezo duniani Cas ambapo Shirikisho hilo la soka lilipaswa kumlipa kocha huyo dola milioni 109 kama fidia baada ya kutomlipa stahiki zake na hivi sasa Fkf imeongezewa siku 30 zaidi kulipa na kila malipo yatakayofanyika Fifa itajulishwa.

Endapo Shirikisho hilo litashindwa kulipa basi litaondolewa kwenye michuano hiyo ya awali kuwania kufuzu kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022 adhabu sawa na waliyopewa Zimbabwe mwaka 2018.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka