Connect with us

Makala

Yanga Princess Yaibuka Mbabe Kwa Simba Queens

Klabu ya wanawake ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua alama tatu muhimu mbele ya Simba queens baada ya kuifunga kwa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake nchini uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam.

 

Yanga Princess imepata ushindi huo muhimu mbele ya Simba queens na kufanya sasa iwe imepata ushindi wa pili katika michezo 13 iliyozikutanisha timu hizo ambapo Simba queens imeshinda michezo tisa na sare mbili.

Bao pekee katika mchezo huo lilipatikana dakika ya 49 likifungwa na Jeannine Mukandayisenga akipiga shuti lililojaa wavuni moja kwa moja ambapo juhudi za kusawazisha hazikuzaa matunda kwa Simba queens.

Yanga Princess kwa miaka ya hivi karibuni wamezidi kuimarika hasaal tangu kocha Edna Lema arejee klabuni hapo ambapo wamefanya sajili za maana zinazosaidia timu kupata matokeo.

Baada ya kupata ushindi huo sasa Yanga Princess wamefikisha alama 30 katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu ya Wanawake nchini huku Simba queens pamoja na kufungwa bado wapo kileleni wakiwa na alama 34.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala