Connect with us

Makala

Simba Sc Yampiga Pini Karabaka

Klabu ya Simba Sc leo imeondoka kuelekea mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya klabu ya Namungo Fc  utakaopigwa siku ya jumanne katika  uwanja wa Majaliwa stadium.

Kwenye mchezo huo Namungo Fc itamkosa kiungo wake Saleh Karabaka ambaye alisajiliwa kwa mkopo kutoka Simba na mkataba wao unasema hawezi kucheza mchezo dhidi ya Simba.

Karabaka ameitumikia Namungo kwenye michezo mitatu [3] ametoa pasi mbili [2] za mabao huku akiwa hajaonja ladha ya kufunga goli.

Vifungu hivyo vya kumzuia mchezaji kucheza dhidi ya timu yake inayommliki imekua ni kawaida katika ulimwengu wa soka ukiwa na lengo la kulinda mbinu za kiufundi ambazo mara nyingi mchezaji huyo anakua anazifahamu kutokana na kuitumikia klabu husika.

Simba sc katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini mpaka sasa ina alama 47 ikicheza michezo 18 ya ligi kuu katika nafasi ya pili huku Namungo Fc yenyewe ikiwa na alama 21 katika nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi kuu ikicheza michezo 19 mpaka sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala