Klabua ya Simba sc imeshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya African Football League baada ya kutoka sare ya 1-1 na Al Ahly katika mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali uliofanyika nchini Misri.
Katika mchezo wa awali siku ya ijumaa wiki iliyopita jijini Dar es salaam timu hizo zilitoka sare ya 2-2 hivyo kuifanya Simba sc kuhitaji ushindi ama sare ya kuanzia 3-3 ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mipya ambayo inajumuisha timu nane pekee.
Wengi wameonyesha kushangazwa na kiwango cha Simba sc katika mchezo huo wa ugenini baada ya kuonyesha kiwango imara sana hasa katika safu ya kiungo na ulinzi huku wakisaidiwa na kukosekana kwa utulivu kwa washambuliaji wa Al Ahly Fc ambao walitengenezewa nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo.
Wakianza na kikosi kilicgokua na mabadiliko machache kama kile cha mchezo wa kwanza ambapo John Bocco na Sadio kanoute walianza badala ya Mzamiru Yassin na Luis Miqqueson huku golini akianza Ally Salim akisaidiwa na mabeki Mohamed Hussein,Shomari Kapombe,Henock Inonga na Che Fondoh Malone huku eneo la kiungo Kanoute,Fabrice Ngoma,Saido Ntibanzokiza na Cletous Chama wakianza sambamba na Kibu Dennis.
Simba sc walishangaza wenyeji baada ya kupata bao la kichwa likifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 68 ya mchezo lakini utulivu wa Al Ahly uliwasaidia kwani walisawazisha bao hilo dakika ya 76 kupitia kwa Mahmoud Kahraba.
Baada ya dakika 90 kumalizika na Al Ahly kufuzu kwa faida ya bao la ugenini ambapo wanatarajiwa kukutana na Mamelod Sundowns ambao nao wamefuzu wakiwafunga 2-0 timu ya Petro de Luanda ya Angola.