Connect with us

Makala

Musonda,Yanga sc Mambo Fresh

Taarifa kutoka nchini Zambia zinadai kwamba Klabu ya Yanga ipo mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji Kennedy Musonda kutoka klabu ya Power Dynamos ya nchini humo kwa dau dola laki moja ambazo ni zaidi ya  shilingi milioni 230 za kitanzania.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Zambia mwenye umri wa miaka 29, msimu huu amefunga jumla ya magoli 11 katika mechi 17 alizocheza na alikua na ofa kubwa ya kujiunga na klabu za Tp mazembe na Simba sc lakini taarifa zinadai kuwa Yanga sc imefanikiwa kushinda mbio hizo.

Staa anatarajiwa kuwasili nchini wiki ijayo tayari kukamilisha dili hilo ambapo anakuja kusaidiana na mshambuliaji Fiston Kalala Mayele katika eneo la mbele huku Heritier Makambo akitajwa kuwa ataondoka klabuni hapo kumpisha baada ya kushindwa kuonyesha makeke tangu asajiliwe na kumuachia ufalme Mayele.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala