Wednesday, May 7, 2025
Home Makala Saido Mambo Fresh Geita Sc

Saido Mambo Fresh Geita Sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza tayari amekamilisha taratibu zote kuitumikia klabu ya Geita Golds Sc iliyomsajili kwa ajili ya kuitumikia msimu huu baada ya kuachana na klabu ya Yanga sc msimu uliopita.

Saido amesajiliwa kama mchezaji huru kuja kuiongezea nguvu klabu hiyo hasa katika michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho ambayo klabu hiyo inashiriki pamoja na Azam Fc huku Yanga sc na Simba sc wakishiriki katika michuano ya klabu bingwa.

Awali Geita Gold sc ilishindwa kumtumia mchezaji huyo katika michezo mbalimbali kutokana na usajili wake kutokamiliki hasa baadhi ya taratibu muhimu ambapo sasa kila kitu kimekaa sawa kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo Hemed Kivuyo.

banner

“Saido Ntibazonkiza ni mchezaji wetu kuna vitu vilikua havijakaa sawa tayari tumeviweka vizuri na mechi ijayo ya ligi kuu anaweza akacheza kama mwalimu Minziro atampa nafasi ya kucheza” Alisema Afisa Habari huyo ambaye pia ni moja ya watangazaji wa Televisheni waandamizi.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.