Connect with us

Makala

Mgunda Anukia Coastal Union

Klabu ya Coastal Union yenye makazi yake jijini Tanga imeripotiwa kuwa ipo mbioni kumrejesha kocha Juma Mgunda kuifundisha klabu hiyo baada ya kuachana nayo kumpisha Mbrazil Melis Medo.

Awali klabu hiyo msimu uliopita ilikua chini ya Mgunda ambaye alitimuliwa na kuajiriwa Mbrazil Melis Medo ambaye naye hakudumu muda mrefu na kuamua kuachia ngazi huku sababu mbalimbali zikitajwa ikiwemo kukosa maelewano na viongozi wa juu wa klabu hiyo ambapo kwa muda timu ilikua chini ya kocha msaidizi Joseph Lazaro.

Inadaiwa sasa tayari Mgunda alishakubali kurejea klabuni hapo huku akitarajiwa kuanza kazi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba sc utakaofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini humo mwezi Aprili.

Mgunda ni moja ya makocha wazoefu wa Kitanzania ambapo pia amewahi kujumuishwa katika benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) akiwa kama mmoja ya makocha wasaidizi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala