Connect with us

Makala

Mashabiki Wafurahi Sawadogo Kutemwa

Mashabiki wengi wa klabu ya Simba sc wamefurahishwa na kitendo cha klabu hiyo kuamua kuvunja mkataba na kiungo wa klabu hiyo Ismael Sawadogo kutokana na staa huyo kuonyesha kiwango duni tangu asajiliwe katika dirisha dogo mwezi januari mwaka huu.

Mashabiki hao wameonyesha kufurahishwa na suala hilo wakitaka sasa nafasi hiyo ijazwe na kifaa cha maana cha kimataifa ili kuwapoza machungu ya kukosa ubingwa wa ligi kuu kwa miaka miwili mfululizo.

Shabiki mmoja aitwaye shabani Juma mkazi wa Tungi jijini Dar es salaam yeye alisema kuwa “afadhali klabu imemtema kwa maana hakua na msaada wowote tangu asajiliwe huku akionekana kuwa ni mzito”alisema shabiki huyo.

Pia hata ukipita katika baadhi ya vijiwe vya kahawa maeneo mbalimbali nchini baadhi ya mashabiki walifurahishwa na kutemwa kwa staa huyo huku wakiuomba uongozi wa klabu hiyo kuwa makini katika kusajili ili kuepuka kusajili magarasa.

Ismael Sawadogo ameitumikia Simba Sc kwa miezi 6 tu huku akicheza Michezo 4 tu ambapo waajiri wake Simba Sc wamevunja Mkataba nae kwa kutoridhishwa na Kiwango chake ambapo alikua anawekwa benchi mara kwa mara huku eneo la kiungo likibaki kwa Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala