Connect with us

Makala

Eng.Hersi Apangua Uongozi Yanga sc

Rais wa klabu ya Yanga sc Eng.Hersi Said aliyechaguliwa hivi karibuni ameanza kuipangua safu ya uongozi wa klabu hiyo ili kutengeneza safu yake ambayo atashirikiana nayo katika kipindi chake cha uongozi.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari ya klabu ya Yanga sc inaonyesha kuwa Rais huyo kwa kushirikiana na kamati ya utendaji tayari imewateua Saad Kawemba kuwa mkurugenzi wa mashindano ya klabu hiyo akichukua nafasi ya Thabit Kandoro ambaye mkataba wake umefikia tamati.

Huku pia akimteua Walter Harrison kuwa Meneja wa timu akichukua nafasi ya Hafidh Salehe ambaye ameteuliwa kuwa maratibu wa timu na mabadilik0 hayo yanalenga kuongeza tija kwa timu hiyo.

Hersi amekua katika mchakato mgumu wa kuunda safu yake ya uongozi klabuni hapo ambapo taarifa za ndani zinasema kuwa Taji Liundi anaweza kwenda kushika nafasi ya Hassan Bumbuli kama mkuu wa idara ya Habari ya klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala