Bodi ya ligi kuu nchini imetangaza ratiba ya michezo mbalimbali ya ligi kuu ya Nbc nchini iliyosalia mpaka kumalizia msimu huu wa 2024-2025 ambapo mechi baina ya Yanga sc dhidi ya Simba Sc iliyokua imeghairishwa kufanyika Juni 15 2025.
Mchezo huo namba 184 uliahirishwa na bodi ya ligi kuu nchini kutokana na klabu ya Simba Sc kugoma kuleta timu uwanjani kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuzuia kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo.
Ratiba hiyo mpya iliyotolewa mapema leo imeonyesha kuwa michezo mbalimbali ya ligi kuelekea mwishoni mwa msimu huu itachezwa kwa wakati mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi juni ambapo ligi itakua imeisha ambapo pia kombe la Shirikisho la Crdb nao litakua ukingoni.
Hata hivyo bado sintofahamu inaendelea kuhusu kufanyika kwa mchezo huo uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11 jioni ambapo mpaka sasa msimamo wa klabu ya Yanga sc ni kutocheza mchezo huo wakianisha kuwa kanuni hazikufuatwa katika kuahirisha mchezo wa awali.