Connect with us

Makala

Nabi Afungiwa Mechi 3

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga sc Nasreddine Mohamed Nabi amkumbana na adhabu ya kukosa michezo mitatu na faini ya kiasi cha shilingi laki tano baada ya kuwashambulia kwa maneno waamuzi wakati wa mchezo baina ya klabu yake na Ihefu uliomalizika kwa Yanga sc kupoteza kwa 2-1 na kumaliza mwendo wa kucheza michezo 49 bila kufungwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya ligi kwa vyombo vya habari adhabu ya kocha huyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 42:2(2.1) kuhusu udhibiti wa makocha.

Nabi kufuatia adhabu hiyo anatarajiwa kukosa michezo mitatu ijayo ya klabu yake ambayo itavaana na Prisons siku ya Jumapili huku ataukosa mchezo dhidi ya Namungo Fc utakofanyika mjini Ruangwa na ule wa kombe la shirikisho dhidi ya Kurugenzi Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala