Tuesday, May 6, 2025
Home Makala Inonga Majanga Tupu

Inonga Majanga Tupu

by Sports Leo
0 comments

Beki wa kati wa klabu ya Simba sc Henock Inonga ameendelea kuwa na msimu mbaya baada ya kuumia katika mchezo unaoendelea wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union na kulazimika kupelekwa hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa.

Tukio hilo limetokea dakika ya 20 ya mchezo wakati Simba ikicheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika Uwanja wa Uhuru huku ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0 mpaka kipindi cha kwanza yote yakifunga na Jean Baleke.

Wakati Inonga akiwania mpira akakutana na Ugando na kusababisha ajali hiyo na mshambuliaji huyo akapewa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi, Ahmed Arajiga huku haraka baada ya kupewa huduma ya kwanza alilazimika kukibizwa hospitali.

banner

Huu unaweza kuwa msimu mbaya zaidi kwa staa huyo raia wa Congo Drc baada ya kutoka majeraha ya bega alipoumia katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Singida Fountain Gate ambapo alilazimika kukaa nje kwa wiki mbili.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.