Friday, May 9, 2025
Home Makala Azam Fc Yaachana na Kocha Dabo

Azam Fc Yaachana na Kocha Dabo

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc iko mbioni kuachana na kocha wake mkuu Yousouph Dabo sambamba na benchi zima la ufundi la Klabu hiyo kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Dabo pamoja na kudumu msimu mmoja na nusu klabuni na licha ya kutofanikiwa kutwaa taji lolote tangu awasili klabuni hapo bado mabosi wa klabu hiyo waliamini kuwa ipo siku atafanikiwa kuweka historia ya mataji klabuni hapo.

Mabosi wa klabu hiyo walianza kukosa imani na Dabo baada ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Yanga sc katika mchezo wa fainali wa kombe la ngao ya jamii ambapo siku chache baadae akapata ushindi kiduchu wa 1-0 dhidi ya APR katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika na akakubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano jijini Kigali na kuhitimisha safari ya timu hiyo Kimataifa.

banner

Dabo aliweka chumvi kwenye kidonda baada ya suluhu dhidi ya Jkt Tanzania katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Nbc msimu huu na kuwafanya Mabosi kuamua kuhutimisha utawala wake Chamazi.

Mabosi wa klabu hiyo walishaa na Dabo na kukubaliana kuvunja mkataba wake sambamba na benchi zima la Ufundi na sasa kilichobaki na wanakamilisha mambo machache ya kiutawala ili kutangaza kuachana na kocha huyo.

Bado haijajulikana nani atakayechukua jukumu la kukaimu nafasi ya Dabo kwa muda mpaka pale atakapopatikana kocha mpya.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.